HudumaGuide (jina la muda)

Sera ya uhariri

[RASIMU – Peter ahakiki]

Vyanzo

Tunatumia taarifa zinazopatikana hadharani kutoka tovuti na nyaraka rasmi za taasisi za umma. Hatunakili maandishi ya tovuti nyingine; tunaandika kwa maneno yetu na kuweka kiungo cha chanzo rasmi.

Uhakiki

Kila mwongozo una tarehe ya uhakiki wa mwisho na jina la mhariri aliyehakiki. Miongozo hupitiwa upya angalau kila baada ya miezi sita, au mapema zaidi taasisi ikibadilisha utaratibu.

Makosa

Ukiona kosa, tumia kitufe "Ripoti tatizo" chini ya ukurasa. Tunasahihisha haraka iwezekanavyo na tunaweka rekodi ya mabadiliko.

Matangazo

Matangazo yamewekwa alama ya "Tangazo" na hayaathiri maudhui. Hatuweki matangazo karibu na viungo vya kuomba huduma rasmi.