HudumaGuide (jina la muda)

Kuhusu sisi

[RASIMU – Peter ahakiki kabla ya kuchapisha]

HudumaGuide ni tovuti huru inayoeleza kwa lugha rahisi jinsi ya kupata huduma za umma nchini Tanzania: kitambulisho cha NIDA, TIN, usajili wa biashara, vyeti vya RITA, mikopo ya HESLB na nyinginezo.

Tunachofanya

  • Tunaandika miongozo ya hatua kwa hatua kwa maneno yetu wenyewe, kutoka vyanzo rasmi.
  • Kila mwongozo una kiungo cha chanzo rasmi na tarehe ya mwisho ya uhakiki.
  • Picha za skrini ni zetu wenyewe na taarifa binafsi zimefichwa.

Tusichofanya

  • Sisi si serikali na hatuwakilishi taasisi yoyote ya umma.
  • Hatukusanyi ada, hatupokei maombi wala nyaraka.

Tovuti inaendeshwa kwa mapato ya matangazo ili ibaki bure kwa kila mtu.